Shirika la Kulinda Mazingira la Greenpeace, limesema moto unaondelea kuwaka katika Msitu wa Amazon unaharibu Msitu wa Bonde la Kongo barani Afrika na kusababisha matatizo ya kupumua kwa wananchi wa Brazil.
Matatizo ya kupumua hasa kwa watoto yameongezeka kadri moto huo unavyoteketeza eneo hilo na kusababisha idadi ya watu waliotibiwa kutokana na matatizo ya kupumua kuongezeka katika siku za hivi karibuni katika hospitali ya watoto ya Jimbo la Rondonia.