Mjumbe wa amani wa Papa Francis nchini Ukraine atazuru Kyiv Jumatatu na Jumanne wiki hii, kulingana na taarifa kutoka Vatican.
Mwezi uliopita, Papa alimteua Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Bologna na rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, kuongoza ujumbe wa amani wa kumaliza vita nchini Ukraine.
“Ni suala la mpango wenye lengo kuu la kusikiliza kwa kina mamlaka ya Ukraine kuhusu njia zinazowezekana za kufikia amani ya haki na kudumisha ishara za kibinadamu ambazo zinachangia kupunguza mvutano,” ilisema taarifa hiyo.
Wakati wa safari ya kwenda Budapest mwezi wa Aprili, Francis alikutana na mwakilishi kutoka kanisa la Orthodox la Urusi linalounga mkono Kremlin, Metropolitan Hilarion, na kando na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán.
Pia alisikia ushuhuda kutoka kwa wakimbizi, wengi kutoka Ukrainia, na alikutana kando na Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal.