Mjumbe huyo aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mzozo wa Sudan ambao ulizuka kati ya makundi hasimu ya kijeshi mwezi Aprili unaweza kuwa katika hatari ya kuwa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.
Hatua hii inakuja zaidi ya miezi mitatu baada ya Sudan kutangaza kutokubalika kwake baada ya vita kuzuka.
Watu milioni tano wamekimbia makazi yao katika mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi hasimu vya wanamgambo, Rapid Support Forces (RSF).
Katika hotuba yake ya mwisho kwa Baraza la Usalama, Bw Perthes alimkosoa sana mtawala wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na mkuu wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo anayejulikana zaidi kama Hemedti.
Bw Perthes alisema viongozi hao wawili walichagua kuitumbukiza nchi katika vita ambavyo vinaacha historia mbaya ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Aliilaumu RSF kwa unyanyasaji wa kijinsia, uporaji na mauaji katika maeneo inayodhibiti. Pia alilaani wanajeshi wa Sudan kwa mashambulizi ya kiholela ya angani. Alipokuwa akizungumza madaktari katika jiji la Nyala huko Darfur walikuwa wakikabiliana na matokeo ya ukatili mwingine.