June 16 kila mwaka Tanzania inaungana na nchi nyingine za Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo leo June 16, 2017 Makamu wa Rais Samia Suluhu alikuwa Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kinyerezi Wilaya ya Ilala DSM.
“…sote ni wazazi, watoto ni zawadi ya Mungu. Sisi pia tulikuwa watoto na tulitunzwa. Tusingetunzwa tusingekuwa hapa leo. Katika nafasi au hadhi yoyote uliyonayo, tusingetunzwa usingekuwa hapo leo. Hatuna budi kutunza zawadi tunayopewa na Mungu.
“Unapoona jitu zima linakwenda kumdhalilisha mtoto wa kike au wa kiume huyo mtu si mmoja kati yetu. Hafai kukaa ndani ya Jamii yetu. Naomba umchukulie hatua zinazostahiki.
“…kuna udhalilisha wanaofanyiana watoto kwa watoto, wazazi pia tuwe makini katika hilo. Kila mmoja achunge watoto wake. Tuwafundishe watoto wetu. Hata kama mtoto wako ana tabia ya kuwafanyia wenzie, hiyo sio fahari. Huko ni kupotoka na hilo jambo litamchukua mtoto huyo katika akili yake na hatakuwa na maisha mazuri.” – Samia Suluhu.
Zawadi zilizotolewa na Mkemia Mkuu kwa Wanafunzi leo!!!