Leo January 9 2018 stori iliyoshika headlines ni ya Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa kukutana na Rais JPM Ikulu Dar es salaam, baada ya maongezi yao kumeibua mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kumlaumu kwa uamuzi huo.
AyoTV tumemtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ilikufahamu yeye kama kiongozi wa chama hicho anasemaje juu ya suala hilo na msimamo wa chama chake.
Mbowe amesema >>> “Kwanza kumezuka mtafaruku kuhusu ziara ya Lowassa Ikulu leo, hilo kwa upande wa CHADEMA hatuna tatizo ni haki yake ya msingi na alialikwa yeye binafsi, sisi kama chama hatujawahi toa tamko au msimamo wa kuipongeza seriakli ya awamu ya tano,”– Mbowe
JPM IKULU: “Lowassa hakuwahi kunitukana hata siku moja”