Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Magreth Thomas Male mkazi wa kijiji cha Makuyuni Mkoani Arusha,anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumshambilia mume wake anayejulikana kwa jina la Geoffrey John na kumsababishia kifo huku chanzo kikitajwa kuwa ni ugomvi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Makuyunii Ngayo Meyasi,amesema ni kweli tukio hilo limetokea na marehemu alivamiwa nyumbani kwake majira ya usiku na mke wake alipoulizwa alikiri kuhusika na tukio hilo.