Mary Mubaiwa, ambaye tayari anashutumiwa kwa Madai ya Ufisadi, alifikishwa mbele ya Mahakama moja ya Harare na kusomewa mashtaka hayo ya jaribio la Kumuua Mumewe na kisha yeye kukana mashtaka yote
Waendesha mashtaka wanasema, alijaribu kumuua Jenerali Constantino Chiwenga, wakati alipokuwa akipokea matibabu Afrika Kusini miezi sita iliyopita
Jenerali Chiwenga aliyehusika kwa kiasi kikubwa katika kumpindua Rais wa zamani wa Taifa hilo, Robert Mugabe mwaka 2017 anadai kuwa Mary alijaribu kumzuia kupokea matibabu Afrika Kusini
Inadaiwa kuwa, Wakati Chiwenga alipolazwa hospitalini mjini Pretoria, Mary ambaye ni mama wa watoto sita aliutoa mrija wa kumpatia maji (Drip) mgonjwa (Chiwenga) katika mkono wake
Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Dynamos alishawahi kuwa mke wa Shingi Kaondera, mchezaji kandanda aliyeichezea klabu ya Caps.
MAFURIKO DAR: MKASA WA DADA ALIEZAMA NA IST YAKE MTARONI