January 31, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amelieleza Bunge kwamba hadi sasa Ofisi yake imeshamlipia gharama za matibabu pamoja na stahiki zake Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jumla ya shilingi Milion 250 ambapo ametoa onyo la kumtaka Mbunge huyo kuacha mara moja kuendelea kuiongopea jamii kwamba Bunge halijatoa hata senti.
“Bunge hili tumeshamlipa Tundu Lissu jumla ya Shilingi million 250 kwahiyo kuendelea kusema kila mahali kwamba Bunge hili halijampa hata senti moja ni jambo la uongo sana, jambo hili nalitupa upande wake ili akanushe kuhusu hili ili nitoke na mkeka kamili wa kila kitu”-Spika Job Ndugai