Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Kengeja wameshauriwa kuwa raia wema mara wamalizapo muda wao wa kutumikia Chuo cha Mafunzo ili warudi katika jamii na waweze kukubalika pamoja na kuaminiwa kama walivyo raia wengine.
Ushauri huo umetolewa na Mrakibu wa Polisi SP Dkt. Yasin alipofika Chuoni hapo kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo wanafunzi hao ambao wanatumikia chuo hicho kutokana na makosa waliyoyafanya ndani ya jamii.
DKT. Yasin amewataka wanafunzi hao kutambua kuwa, lengo kuu la kuwepo kwao katika chuo hicho ni kurekebishwa tabia zao hivyo amewataka kujutia makosa yao na kudhamiria na kutokurejea tena matendo hayo ambayo hayakubaliki katika jamii na badala yake waje washirikiane na jamii na Jeshi la Polisi kuzuia uhalifu na wahalifu.
Aidha, Dkt. YASIN amesema Jeshi la Polisi halina uadui na raia na wala halifanyi kazi kwa upendeleo au kwa lengo la kumkomoa mtu yoyote bali linafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria zilizowekwa ” Sisi Jeshi la Polisi ni sawa na jamii tunaguswa na kila kundi la watu ndio maana leo tumekuja kuwatembelea na kuwafariji ili msijione kama mmetengwa badala yake mjione kuwa ni sawa na watu wengine walioka katika jamii ” alisema Dkt. Yasin.
Mbali na hayo Dkt. YASIN aliwapatia wanafunzi wa chuo hicho futari ya tende, tambi, maji ya kunywa, sabuni za kufulia na kuongea pamoja na miswaki na dawa za meno.