Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda, amewashangaa watu wanaohoji kitendo cha Rais Magufuli kukutana na Watendaji wa Kata, ambapo amesema kuwa wengi ambao wamekuwa wakihoji walishashindwa kutimiza majukumu yao kwa wananchi.
“Dkt Magufuli alichokiamua hata akitaka kukutana na Wenyeviti wa Mitaa na penyewe mtasema wote anataka wahamie CCM, unajua shida moja tunaruhusu akili ndogo kujadili mambo makubwa, sisi Watanzania wengi tunapoteza sana muda kufikiria vitu kwa njia hasi” Makonda.