Leo July 17, 2019 Kuna hii ya kuifahamu ni kumhusu Mwanamke mmoja mwenye miaka 39 mkazi wa Tanga Kona, Kenya anauguza majeraha baaada ya Mume wake kumnyofoa mdomo na sikio kufuatia ugomvi baina yao.
Jackline Kerubo, Mama mwenye Watoto sita, amesema alitaka kwenda kuchuma mboga katika shamba la jirani yake lakini Mume wake alimkataza.
Jackline anasema Mumewe amefunga nae ndoa miaka 21 iliyopita na kwa sasa anahofia maisha yake pamoja na watoto wake.
Alisema jirani yake aliingilia kati baada ya mume wake kuapa kumpa fundisho. Hata hivyo baada ya kipigo hicho Mume wake alitoweka nyumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari, alisema mume wake alitenda unyama huo akiwa jikoni kwa kumpiga kichwani na baadae kumtafuna mdomo na sikio.
Mkuu wa Polisi Maryline Oundo aliwaomba wanandoa kutafuta ushauri wanapokuwa na mizozo na kuitaka jamii kutoa taarifa za kesi zinazokiuka haki za binadamu ili kupata msaada sambamba na watuhumiwa kuchukuliwa hatua.
Bi Kerubo kwa sasa anapatiwa hifadhi katika kituo cha Polisi Nambale wakati maafisa Polisi tayari wameanza kazi ya kumtafuta mtuhumiwa.
BONGO ZOZO ANATUKANA WAZUNGU KWA KISWAHILI “AFADHALI HAWANIELEWI”