Hiki ni kituo kipya cha daladala ambacho kinafanya kazi baada ya kile kituo cha Mwenge kuvunjwa kwa sasa kupisha ujenzi wa barabara,hivyo wasafiri wote waliokua wanashukia Mwenge na kupandia Mwenge kwa sasa hiki ndicho kituo chao.
Ingawa wasafiri wengi na abiria wamelalamikia hali hii ya Sumatra kuhamisha kwa kituo cha Mwenge kupelekwa Makumbusho lakini tayari kituo hiki kimeshaanza kazi na leo ni siku ya pili.