Katika kuonyesha moyo wa mawingu Ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara imekabidhi mifuko 400 ya Saruji ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa mkuu wa mkoa huo mnamo Dec 30, 2023 ya kutoa msaada huu kwa waathirika wa Maporomoko ya tope wilani Hanang Mkoani Manyara.
Akikabidhi msaada huo kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhandisi Juma Kandoro amesema mifuko hiyo, imetokea na mdau wa maendeleo kwa ushikiano wa mkuu wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni ahadi aliyoitoa Dec 30 Mwaka jana.
Akipokea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara Bi Janeth Mayanja ambaye ni mkuu wa wilaya ya Hanang, ameishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara kwa kuendelea kuonyesha moyo wa utoaji pamoja na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kurejesha maisha ya wananchi wa Hanang’ walioathirika.