Ripoti za hivi punde kulingana na Sky News jeshi la magereza la Urusi limeripoti kuwa mkosoaji na mpinzani wa Putin Alexei Navalny amefariki.
“Mnamo Februari 16, 2024, katika koloni nambari 3, mfungwa A A Navalny alijisikia vibaya baada ya kutembea, na kupoteza fahamu mara moja,” taarifa inasema.
“Wahudumu wa matibabu wa taasisi hiyo walifika mara moja na timu ya matibabu ya dharura iliitwa.
“Hatua zote muhimu za kurudisha uhai wake zilifanywa, lakini hazikutoa matokeo chanya.
“Madaktari wa dharura walithibitisha kifo cha mfungwa huyo,” ilihitimisha.
Licha ya hatari zilizo mpata Bw Navalny alikamatwa na kupatikana na hatia kwa mashtaka ambayo anasema yanachochewa kisiasa, na kusalia katika magereza ya Urusi hadi kifo chake kiliporipotiwa leo.