Leo April 30,2018 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam imetoa Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya mkopo kwa wakina mama na vijana.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati wa kutoa mikopo hiyo, Meya Boniface Jacob amesema mikopo hiyo itatolewa kwa watu wa Ubungo na sio kwengine.
Pia Meya Jacob ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwani idadi yao imeonekana kuwa ndogo kwani mfuko huu ni nusu kwa vijana na nusu kwa kina mama na asilimia 20 inakwenda kwa walemavu.
BREAKING: Mahakama yaamuru Hans Poppe wa Simba SC akamatwe