Tuchel alishinda taji la Bundesliga akiwa na wababe hao wa Bavaria msimu uliopita lakini timu yake kwa sasa inawafuata viongozi wa ligi hiyo Bayer Leverkusen kwa pointi tano baada ya kushindwa 3-0 na vijana wa Xabi Alonso.
Taarifa zinasema kocha wa sasa wa Barca Xavi Hernandez anaacha nafasi yake mwishoni mwa msimu huu.
Gazeti la The Sun limeandika: “Thomas Tuchel ameripotiwa kujipendekeza kwa Barcelona huku kukiwa na shaka juu ya mustakabali wake wa Bayern Munich.
Kutakuwa na nafasi katika Barcelona msimu huu wa joto baada ya Xavi Hernandez kutangaza nia yake ya kujiuzulu kutoka kwa dimba.
“Hata hivyo, mshindi huyo wa Ligi ya Mabingwa tayari anasemekana kupanga hatua yake nyingine.