Ni June 8, 2023 ambapo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, Plasduce Mbossa amefanya mahojiano katika kituo cha Clouds Media Group kuelezea sakata linaloendelea mitandaoni juu ya Bandari ya Dar es Salaam.
“Kuna mtu anakwambia Bandari imeuzwa kuna sehemu ipi ya Tanzania iliwahi kuuzwa? Je kuna utaratibu wa kuuza?- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
“Kwa kawaida bandari inapofanya kazi hata zile tozo humtozi kwa faida unamtoza yaani kwamba umetumia mafuta kiasi gani, umenunua mitambo kiasi? Au ule uwekezaji kume-maintain gati gharama zake kiasi gani? Unaivunja kidogo kidogo unamtoza mteja mmoja mmoja lakini Mamlaka ya Mapato yenyewe ndio inakusanya fedha”- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
“Ukiwa na meli nyingi na mzigo mwingi ambao utapitishiwa kwako na ukawa inalipa Kodi au hata ambao unakwenda nje utasafirishwa na malori ambayo yanalipa kodi yenyewe nakusajiliwa hapa. Maana yake ni kwamba mamlaka yetu ya Mapato itakusanya zaidi kupitia bandari zetu” Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)