Katika kudhibiti ubora na Usalama wa Vipodozi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hutumia viwango vya bidhaa husika na miongoni mwa viwango hivyo ni kiwango cha lazima (compulsory Standard) namba TZS 638:2014, ambacho pamoja na na mambo mengine kimeeleza viambato vinavyoruhusiwa kutumika kwa kiasi maalum na vile visivyoruhusiwa kabisa katika uzalishaji wa vipodozi.
Ameyasema hayo leo Mei 17,2022 Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dkt.Athuman Ngenya wakati akifungua mkutano kati ya TBS na wadau wa vipodozi katika ukumbi wa mikutano TBS Jijini Dar es Salaam.
Amesema kwaa mujibu wa tafiti zilizofanyika hivi karibuni juu ya viambato ambavyo vinaruhusiwa kutumika kwa masharti ya kiasi maalumu, imebainika kwamba matumizi ya muda mrefu ya baadhi ya viambato hivyo yanaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji na hivyo kufikia uamuzi wa kuzuia matumizi ya viambato hivyo katika utengenezaji wa vipodozi.
“Viambato vilivyozuiwa vinafahamika kwa majina ya Zinc pyrithione, Butyphenyl methypropional na Sodium hydroxymethylglcinate”. Amesema Dkt.Ngenya.
Aidha Dkt.Ngenya amesema pamoja na zuio hilo, Shirika limeona ni vyema zaidi kukutana na wadau husika kuweka uelewa wa pamoja kwa manufaa ya nchi na kuepusha madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya bidhaa zenyeviambato hivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dkt.Athuman Ngenya akisistiza jambo wakati akifungua mkutano kati ya TBS na wadau wa vipodozi uliofanyika leo Mei 17,2022 katika ukumbi wa mikutano TBS Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika mkutano kati ya TBS na wadau wa vipodozi uliofanyika leo Mei 17,2022 katika ukumbi wa mikutano TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Gervas Kaisi akizungumza katika mkutano kati ya TBS na wadau wa vipodozi uliofanyika leo Mei 17,2022 katika ukumbi wa mikutano TBS Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa Vipodozi wakiwa kwenye mkutano na Shirika la Viwango Tanzania TBS kujadili masula mbalimbali yyanayohusu vipodozi, mkutano umefanyika leo Mei 17,2022 katika ukumbi wa mikutano TBS, Jijini Dar es Salaam