Mkurugenzi wa hospitali kubwa zaidi ya Gaza amekamatwa na Jeshi la Ulinzi la Israel, wizara ya afya inayoongozwa na Hamas imesema.
Dk Selmeya alizuiliwa pamoja na wafanyakazi wa matibabu katika al Shifa, msemaji wa wizara hiyo alisema.
Kituo hicho kimekuwa lengo kuu la operesheni ya ardhini ya Israel kaskazini mwa Gaza, huku wanajeshi wakiivamia wiki iliyopita.
IDF imedai Hamas inatumia eneo la chini ya hospitali kufanya mashambulizi na kuwaficha mateka – madai ambayo kundi la wanamgambo limekanusha.
“Dkt Selmeya, mkurugenzi wa Hospitali ya Al Shifa, pamoja na baadhi ya wahudumu wa afya ambao bado wapo katika hospitali hiyo, wamekamatwa,” Dk Ashraf al Qudra alisema.