Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amejiweka Karantini baada ya mtu mmoja aliyepatikana na CoronaVirus kumtaja kama mmoja wa watu wa karibu aliokutana nao.
Amesema, “Nimetajwa kama mmoja wa watu waliokutana na mtu aliyepatikana na COVID19. Nipo vizuri na sina dalili lakini nitajiweka karantini kwa siku zijazo, kwa mujibu wa taratibu za WHO, nikifanya kazi kutokea nyumbani”.
Tedros ameongeza kuwa ni muhimu kwa watu wote kufuata taratibu za kiafya zinazotolewa kwani kufanya hivyo kutavunja mnyororo wa maambukizi ya COVID 19, kuvizidi nguvu na kulinda mifumo ya afya
Kauli ya Tedros inakuja wakati Mataifa Barani Ulaya kama vile Switzerland na Uingereza yakiingia katika kipindi kipya cha Karantini kufuatia ongezeko la maambukizi.
UWEZO WA MAKOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI