Huduma za dharura za Urusi zimesema kuwa miili ya abiria wote kumi kwenye ndege ya Embraer Legacy sasa imepatikana.
Kulingana na mamlaka, waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ni pamoja na bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin na kamanda wake wa pili Dmitry Utkin – mtu ambaye alipatia kundi hilo la mamluki jina lake.
Juhudi sasa zinaelekezwa kubaini juu ya kile kilichosababisha ajali hiyo.
Polisi wameziba eneo karibu na eneo la ajali na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Urusi imeunda tume maalum kuchunguza hilo.
Wakati Prigozhin ilipoanzisha uasi ulioshindwa miezi miwili iliyopita, pia alipinga mamlaka ya Vladimir Putin mwenyewe. Na hilo ni jambo ambalo Rais wa Urusi hawezi kulisahau kirahisi.
Article share tools
Warusi wengi hawakushangaa wakati taarifa za kifo cha Prigozhin ziliripotiwa jana.