Afisa mkuu wa mawasiliano wa Manchester United Toby Craig amekiri kuwa wamiliki hao hawajafurahishwa na mwanzo mbaya wa timu hiyo katika msimu mpya.
Kumekuwa na uvumi mwingi juu ya mustakabali wa meneja Erik ten Hag baada ya United kuanza vibaya zaidi katika historia ya Premier League katika kampeni za 2024-25. Hadi Jumamosi iliyopita waliposhinda 2-1 nyumbani dhidi ya Brentford, Mashetani Wekundu walikuwa katika nafasi ya 14 kwenye ligi na walikuwa wamefanya mechi tano bila ushindi katika mashindano yote.
Kundi la INEOS, linaloongozwa na Sir Jim Ratcliffe, na familia ya Glazer walifanya mkutano wa bodi wakati wa mapumziko ya kimataifa kujadili mustakabali wa kocha huyo Mholanzi. Ingawa mkutano huo haukutoa maamuzi yoyote makubwa, afisa mkuu wa mawasiliano wa Red Devils Tony Craig amefichua kwamba wamiliki hawajafurahishwa haswa na mwanzo mbaya wa timu msimu huu.