Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila anafanya ziara mchana na usiku ya kukagua Barabara, Madaraja yaliyoharibiwa na mvua ili kuhakikisha wananchi wanapita katika maeneo hayo haraka iwezekanavyo
Akiwa katika Daraja la Mbopo lililokuwa limekatika Mhe. Mkuu wa Mkoa amekuta hatua za haraka zimeshachukuliwa ambapo daraja lenyewe liko Imara Ila kingo za udongo ndio zilizoliwa na kupelekea kuagiza kuwa ifikapo saa tano ya leo Daraja Hilo Liwe linapitika kwa watu wote ili kuondoa usumbufu
Hata hivyo RC Chalamila alipofika katika Daraja la Tanganyika alikuta Daraja Hilo limeathirika kutokana na mabadiliko ya mto ambapo watu wanafanya Shughuli kwenye mto hivyo mto kubadili njia na kupita sehemu tofauti na Daraja lilipo ambapo napo alikuta kazi ikiendelea na kupata uhakika kutoka kwa Meneja wa TARURA kuwa ndani ya siku tatu wananchi watakuwa wanapita
Vile vile Mhe. Mkuu wa Mkoa akawataka wenye nyumba zilizovamia mto, walioko mabondeni na wanaofanya Shughuli za kibinadamu kwenye Mito kuondoka Mara moja katika maeneo hayo kwa kuwa ni maeneo hatarishi
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Injinia Geofrey Mkinga amekili kupokea maagizo yote na kuahidi kuyafanyia kazi