Ni Agosti 4, 2023 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Anthony Mtaka ametembelea mabanda ya maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya,
katika Maonesho hayo pia ametembelea banda linalohusika na uuzaji wa gasi, Lake Energies Group ambapo baada ya kufika alinunua na kukabidhiwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group Matina Nkulu.
Aidha akizungumza na millarday.com & Ayo TV Meneja Masoko wa Lake Energies alisema… ‘Kwanza ningependa kuwashukuru kwa kunipatia fursa hii ya kipekee na pia kuwashukuru waratibu wa maonesho ya Nanenane kwa kutupa nafasi ya kuja kutoa Elimu juu ya Nishati ya Gasi, tuliona siku za nyuma Waziri mwenye dhamana kwenye Wizara ya Nishati Mh. January Makamba alishaimba na kupita baadhi ya mikoa akisisitiza juu ya utumiaji wa Nishati ya Gasi kwa maana Wananchi waache kutumia kuni sasa ipo Gesi ya bei nafuu ambayo ni Lake Energies itakayomuwezesha mtanzania kutumia katika matumizi yake ya kila siku hususani pale anapokuwa nyumbani’- Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group Matina Nkulu.
‘Kwahiyo Elimu hiyo hiyo bado inaendelea na ndio maana tuko hapa katika viwanja vya Nanenane ili kuuza na kutoa Elimu juu ya utumiaji wa Nishati ya gesi’- Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group Matina Nkulu.
‘Lengo letu sisi Lake Energies Group ni kumtua mama Kuni kichwani ndio maana tunataka Watanzania wote hususani waishio kijijini hata mijini Elimu iwafikie hakika Lake Energies ni yetu sote’– Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group Matina Nkulu.