Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma (TAKUKURU) inamshikilia Baraka Sabi mwenye umri wa miaka arobaini na moja (41) ambaye ni Mkuu wa Shule Sekondari Serengeti iliyopo Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kwa msichana ( jina limehifadhiwa) Mkazi wa kata ya Hazina Jijini humo.
Akizungumza na waandishi na habari leo ofisi kwake Jijini Dodoma Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo Sostenes Kibwengo amesema Desemba 12 , 2019 TAKUKURU ilipokea taarifa kutoka kwa Msichana huyo ambaye alihitimu kidato cha Sita katika Sekondari ya Serengeti mwaka 2016 huku akidai mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sera ya 329 Marejeo ya Mwaka 2019.
MILLARD AYO NA MASTAA WA BONGO WAPEWA KAZI MOJA TU NA TANAPA