Leo April 25, 2018 Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeingia kwenye historia mpya ya kuanza kupokea meli kubwa yenye urefu wa mita 264 aina ya Northern Power kwenye bandari ya DSM ambapo awali meli zenye ukubwa huo hazikuweza kutia nanga kwenye bandari hiyo na kutoa fursa kwa bandari za Durban Afrika Kusini na Mombasa nchini Kenya.
Juhudi za kuongeza uwezo Bandari ya DSM sasa zimewezesha meli kubwa kutia nanga na kuiwezesha Tanzania kuingia katika ushindani wa meli kubwa kwa sababu wasafirishaji wa mizigo yenye ujazo mkubwa upendelea kutumia meli kubwa ili kupunguza gharama za kusafirisha mizigo mara kwa mara.
Meli hiyo inapita maeneo mbalimbali dunia kusambaza mizigo imewasili nchini makontena 5063
Akizungumza Bandarini DSM Mkurugenzi wa shughuli za Meli, Yusuph Mwingamno amesema “Wasafrishaji wa meli wanapenda kutumia meli kubwa kuepuka gharama, nikiwa na maana kwamba Mombasa na Durban wao bandari zao ni kubwa wanaingiza meli kubwa kuliko zinanzoingia DSM, maanake ni kwamba wafanyabiashara wengi watakuwa wanachukua mizigo nje wanapeleka kwao, halafu sisi tuchukue kwao kwa vimeli vidogo na vimeli vidogo vinalipa kidogo”
Ujio Mpya: Miss Arusha jinsi ya kushiriki na tarehe ya shindano