Msemaji wa polisi nchini humo Lawan Shiisu Adam amesema hadi sasa wamethibitisha vifo vya watu 94 huku kionya kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.
Polisi wameendelea kueleza kuwa wengi wa walioathiriwa walikuwa wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika baada ya lori kuanguka jana jioni katika mji wa Majia jimboni Jigawa.
Chama cha Madaktari nchini Nigeria kimewataka wahudumu wa afya kuwasili haraka kwenye vituo vya dharura vilivyo karibu ili kusaidia kutoa huduma kwa idadi kubwa ya majeruhi.
Ajali kama hizi zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini Nigeria na kusababisha vifo vya watu mamia ya watu.