Leo March 26, 2018 Mama mdogo wa marehemu Allen, kijana aliefariki Mbeya baada ya kushikiliwa na Polisi amesema kijana huyo alikamatwa na kupelekwa Polisi kutokana na kuwaambia wenzake wakimbie baada ya kuwaona Polisi wanakuja.
“Marehemu aliekua muuza machungwa Ijumaa alikwenda ktk lile libeti la kichina akawaona Maaskari, baada ya kuwaona akawaambia wenzake wakakimbia yeye akabaki, wakamkamata kwanini amewaambia wenzake” -Mama mdogo wa Allen
Nae Bibi yake Allen ameongea kuhusu tukio amesema “Mjukuu wangu ameuawa bila hatia kwani alikuwa si mlevi wala mvutaji wa bangi nawashangaa Polisi kupiga mabomu tukiwa msibani.”
Vurugu ziliripotiwa Airport ya zamani Mbeya usiku wa March 25 ambapo chanzo ni kifo cha Allen ambapo Polisi walipotafutwa walitoa ufafanuzi ufuatao kuhusu tukio hilo
“Vurugu Airport ya zamani inahusiana na oparesheni tunayofanya ya vibaka wanaokaba usiku, Katika watuhumiwa mmoja alidhaminiwa alipofika nyumbani alionekana anaumwa na jioni akafariki lakini haihusiani na kwamba kapigwa kituoni” -RPC Mpinga
“Msako huu utaendelea mpaka hali itakapo tulia, lazima tuhakikishe panakuwa salama, Mabomu ni kawaida unapotaka kutawanya watu sio silaha za moto na hayajaleta madhara yoyote, hatuwezi tumia silaha za moto kuwatawanya tunatumia mabomu”-RPC Mpinga