July 27 2016 Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimekutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kuzungumzia suala la serikali kupiga marufuku mikutano ya vyama huku wakidai ni kunyimwa haki yao ya kimsingi ya kuzungumza.
Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema…>>>’Serikali kupitia Waziri mkuu na hatimaye Rais na jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka 2020 ili kuipa Serikali nafasi ya kufanya kazi’
‘Huu ni ukiukwaji wa ibara ya 20(1) ya katiba, aidha katazo la mikutano ya siasa inakiuka sheria namba 5 ya vyama vya siasa mwaka 1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya kazi ya siasa‘ –Freeman Mbowe
ULIIKOSA HII POLISI KUHUSU TAMKO LA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA TANZANIA