Mmiliki mmoja wa duka la noodles [tambi]anachukulia desturi hii kwa uzito sana hivi kwamba alianza kupanga muda ambao wateja wake wangechukua kuanza kula na kumaliza.
Aligundua kwamba wale ambao walitumia muda mrefu zaidi wakati wa kula chakula hicho walikuwa wakitazama video kwenye simu zao, na kuwafanya washindwe kufanya jambo moja au lingine kwa wakati mmoja au wakati sahihi.
Kota Kai anamiliki na kuendesha mgahawa wa Tokyo Debu-chan ambayo itaadhimisha mwaka wake wa tano Juni hii.
Mnamo Machi, aliamua kupiga marufuku wateja kutumia simu zao za mkononi wakati wa kula hatua ambayo ikawa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Japan.
Mmiliki huyo wa mgahawa anasema tambi nyembamba anazotoa zina upana wa milimita moja tu, hivyo huanza kupoa na kuharibika kwa haraka sana kwa mantiki hiyo, kusubiri kwa dakika nne kunaweza kusababisha mlo mbaya.
“Viti vinapojaa naona watu wanaacha kula huku wakitizama simu zao za mkononi, nawaambia waache,” Kai anasema.
Anaongeza kuwa hajaweka alama zozote za kuwataka watu waweke simu zao badala yake, anazungumza na wateja mmoja mmoja.
Kwake, rameni [tambi] ni zaidi ya chakula tu.
“Ninahisi ni burudani ambayo lazima ijumuishe sheria,ni kama ‘unapokuwa Roma, fanya kama Waroma wanavyofanya.’ Chalula aina ya Ramen ni aina ya tafrija.’”
Debu-chan sio mahali pa kwanza kushughulikia matumizi ya simu wakati wa kula.
Mgahawa mmoja wa McDonald huko Singapore kiliwahi kuendesha “Zima simu , Burudani inaendelea.” kampeni mwaka wa 2017 ya kuzima simulator wakati wa kula.
Mgahawa huu uliweka makabati maalum ya kuhifadhia simu ambapo wateja wangeweza kuweka simu zao wakati wa kula, lengo likiwa ni la watu kutumia muda mwingi wakati wa kula na familia hasa watoto wao.
Katika migahawa ya tambi ya nchini Japani, kuna sheria ambayo haijatamkwa mbayo ni ‘kula haraka na kuondoka’.