Bilionea wa Uingereza Hamish Harding ambaye ni mmoja kati ya Watu watano waliofia baharini katika ajali ya chombo cha majini walichokua wakisafiria kwenda kutazama mabaki ya Meli ya Titanic, alipanga kuja kupanda Mlima Kilimanjaro akiambatana na Familia pamoja na Marafiki zake.
David Mearns ambaye ni Rafiki wa Marehemu Harding, ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza la Sky News kuwa Hamish (58) ambaye alikua Baba wa Watoto wawili alipanga kuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro July mwaka huu, safari ambayo alikuwa na mpango nayo kwa muda mrefu lakini akashindwa kutokana na janga la corona.
Maafisa wa Ulinzi wa Pwani wamesema vipande vitano vikubwa vya chombo hicho vimepatikana huku mmoja wa waliofariki kwenye ajali hiyo akiwa ni Stockton Rush, Mwanzilishi na Afisa Mkuu wa Kampuni ya OceanGate inayomiliki chombo hicho.