Makamu wa rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, headlines zake zinaendelea kunifikia mtu wangu, naomba ukutane na maneno yake najua utatoka na kitu…leo ni kuhusu wakina mama wajawazito kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
‘Tanzania tumepiga hatua kubwa kwenye malengo ya Millenia lakini tumeshindwa kwenye vifo vya wakina mama wajawazito, tumepiga hatua kubwa kwa watoto tumetoka kwenye zaidi ya watoto 400 kwa vizazi laki moja na tuko kwenye watoto 56 kwa vizazi laki moja….lakini kwa wanawake bado wataalamu naomba tutumie nafasi tunayoweza kujitolea kwa nguvu zetu kunusuru kina mama na vifo wakati wa kujifungua“- Makamu wa Rais Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan.
‘Kujifungua ni kazi takatifu Mungu aliyotupa, hakuna haja ya kufa kwa kufanya kazi hiyo… kifo hakiepukiki lakini tunajitahi kuvipunguza, inasikitisha kwamba yote tumeyaweza lakini hili bado…. nawaomba wataalamu na waziri wa afya muingie ndani muone sababu hasa zinazofanya wakina mama wapoteze uhai wao ili tuzifanyie kazi;- Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.