Leo August 26, 2019 Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi ametangaza baraza jipya la Mawaziri. Baraza hilo limetangazwa hii leo baada ya kusubiriwa kwa miezi Saba.
Katika Serkali hiyo mpya, wanawake wamepewa asilimia 17 ya Mawaziri na wanaume ni asilimia 83, pia imeundwa Wizara maalum ambayo itashughulikia masuala ya watu wenye ulemavu.
Ikumbukwe July mwaka huu Rais Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda Serikali ya muungano itakayokuwa na Mawaziri 66.
SERIKALI YATAJA CHANZO CHA NDEGE KUZUILIWA AFRIKA KUSINI.