Leo June 6, 2018 Kwa mujibu wa ripoti mpya ya serikali ya Uganda inasema kuwa asilimia 60 ya wanafunzi wanaosoma katika shule za msingi nchini humo hawajui kusoma.
Katika ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘The Monitoring Learning Achievement of Primary Two in Literacy’ inasema kuwa kati ya wanafunzi 10 waliohojiwa katika tafiti hiyo 6 kati yao hawajui kusoma.
Aidha ripoti hiyo imebaini kuwa wanafunzi hao wa shule ya msingi wanafanya vizuri sana kwenye kusikiliza tofauti na kusoma.
Kwa upande mwingine serikali ya Uganda imewatupia lawama waalimu wa nchi hiyo kwa kuwapandisha madarasa wanafunzi pasipo kuangalia kwa kina uwezo wao wa kusoma.
Imeripotiwa kuwa ripoti hiyo ilifanywa na waalimu wakuu pamoaja na wasaidizi wake katika muhula wa mwisho wa mwaka 2016 ikichunguza uwezo wa wanfunzi wa shule ya msingi katika Nyanja ya kusikiliza, kusoma, kutofautisha na kulinganisha,kutafsiri na kuandika.