Leo July 31, 2018 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema yeye bado hajaipata Hukumu ya kufunguliwa kwa Gazeti la MwanaHALISI ila ameiona mahali tu na kwamba Kubenea amepotosha mambo mengi wakati anaongea na Waandishi wa Habari.
“Sisi kama Serikali tutatoa taarifa yetu, kama tutakata Rufaa au! nimeisoma Hukumu yote nieleze kusikitishwa na Kubenea amepotosha mambo mengi mno, hata kama Yeye haelewi, bahati mbaya Mwanasheria wake nae alikuwa anajichanganya vitu” Msemaji wa Serikali
LIVE MAGAZETI: Waliomdhalilisha Jokate ”watapata tabu sana”, “Nawasha moto kumchoma Mbowe”