Ni April 5, 2016 ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project).
Akizungumza na waandishi wa habari alisema…>>>’Mradi wa DMDP ni matokeo ya miradi miwili mikubwa inayotekelewa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.Mradi wa kwanza ni ule ujulikanao kama Mradi wa uendelezaji wa miji minane kimkakati (Tanzania Strategic Cities Project – TSCP) unaotekelezwa katika Majiji ya Arusha, Mwanza na Mbeya,Dodoma, Kigoma Ujiji na Manispaa ya Kigoma Ujiji’ – Paul Makonda
‘Madhumuni makubwa ya mradi wa DMDP ni kukabili changamoto zinazolikabili Jiji la Dar es Salaam kwa kutilia mkazo maeneo kama kuboresha huduma za jamii, miundombinu na kujenga uwezo wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam katika utoaji wa huduma za jamii’ – Paul Makonda
‘Kuchangia katika kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi na kusaidia katika kukabili matukio ya dharura kama majanga ambayo yanaweza kulikabili Jiji la Dar es Salaam’ – Paul Makonda
‘Katika mwaka wa fedha 2015/16 Serikali iliingia Mkataba na Benki ya Dunia wenye thamani ya dola za Kimarekani 300 milioni za utekelezaji wa mradi wa DMDP kwa kipindi cha miaka mitano,.Aidha, mfuko wa maendeleo ya nchi za Nordic (NDF) umechangia dola za kimarekani 5 milioni kwaajili ya kukabili changamoto za mabadiiliko ya tabia nchi na Serikali ya Tanzania’ – Paul Makonda
‘Aidha kutekeleza kwa miradi hii itaibadilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam na kutoa muonekano ambao Mhe. Rais ameendelea kutilia msisitizo uwepo wa Miji nadhifu iliyopangwa na yenye mandhari nzuri, hivyo natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dar miradi hiyo itakapokuwa inatekelezwa wailinde na kuitunza kwa maendeleo ya Taifa letu’ – Paul Makonda
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE