Leo July 4, 2018 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile amewataka watafiti nchini kufanya utafiti kwanini wanaume wengi hawapimi UKIMWI.
Dk. Ndungulille ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 6 wa Kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (Muhas).
Dk. Ndungulille amesema takwimu mbalimbali zinaonyesha wanaume hawapendi kupima UKIMWI, hivyo kuna haja ya watafiti kuhakikisha wanapimwa UKIMWI.