Leo May 28, 2018 Ilifanyika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Kigoma Kasuku Bilago katika ukumbi wa Karimjee ambapo Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ameijia juu ofisi ya Bunge la Tanzania kwa kusema kuwa urafiki wao na wabunge wa upinzani ni wamashaka.
Amesema kuwa kitendo cha Ofisi ya Spika wa bunge kutoa taarifa ya mazishi ya Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, Kasuku Bilago kabla ya kufanya mawasiliano na viongozi wa chama kimewashtua sana.
” Ofisi ya Spika inatoa taarifa ya mazishi yake, hili jambo lilitukwaza sana na tukawasiliana kuwaambia wamepanga leo ndio muheshimiwa Bilago aagwe Dodoma, asa huyu wangekuwa wanampenda sana wangemtibu sana, hawana tabia ya kutupenda, wanatabia kututesa” Mbowe