Leo April 20, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amewaapisha Majaji 10, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Ikulu Jijini DSM.
Millardayo.com inakusogezea MAMBO 8 aliyozungumza Rais Magufuli baada ya kuwaapisha Viongozi hao.
“Niliposikia Serikali imeiba TRILIONI 1.5 nikampigia CAG na kumuuliza mbona katika Ripoti uliyoisoma hapa Ikulu sikuona kuwa kiasi hicho kimepotea?, akajibu kuwa hakuna kitu kama hiko, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha nae akasema hakuna” -Rais Magufuli
“Kama Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kipo chini ya Serikali basi kisiachwe bila kuongozwa na kugeuzwa kuwa mali binafsi” -Rais Magufuli
“Sababu ya uhuru wa mtu kuandika chochote na mimi nikacheka tu nikasema hata ndege tuliambiwa ni mbovu, ni kawaida ya uhuru huu” -Rais Magufuli
“Kuna ugonjwa tumeupata sisi Watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao, hii inatokana na sisi kutokui-control mitandao hiyo. Sidhani kama ukienda kwenye nchi kama China kama wana Google na WhatsApp kama tulizonazo sisi” -Rais Magufuli
“Sasa hivi tupo kwenye vita ya uchumi, ni ngumu kweli kweli, ninaamini nimechagua watu wenye qualification zote, sikutaka nifanye kosa, kila mmoja nafahamu” -Rais Magufuli
“Mkaitangulize Tanzania, mtaletewa kesi ngumu, zingine za kudhulumu watoto masikini, hapo ndiyo hekima ya MUNGU inahitajika” -Rais Magufuli
“Kazi ya Jaji ni ngumu kweli kweli, mkamtangulize MUNGU mbele, mtapata vishwawishi vingi, hapa ukute kuna watu tayari wameshajiandaa kukupa rushwa.” -Rais Magufuli
“Kazi ya kumteua Jaji ni ngumu sana, hasa unapomteua ukijua baadae atakuhukumu” -Rais Magufuli
CAG, Katibu Mkuu walivyohojiwa na Rais Magufuli kuhusu TRILIONI 1.5
MAGAZETI LIVE: CAG aibua watumishi hewa, Harusi ya Alikiba yatikisa Afrika Mashariki