Kaimu RPC Mkoa wa Songwe amesema dereva Mawazo Jailozi hakupigwa na Askari wa Usalama Barabarani, bali alikuwa anadhibitiwa kwa kutumia nguvu ya wastani ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Dereva huyo atashtakiwa kwa kumjeruhi Askari na kuzuia maofisa wa TRA kufanya kazi yao.
“Dereva Mawazo aliposimamishwa na Polisi aliwakashfu nakuamua kuondoka, walimfukuzia nakumkamatia Tunduma ambapo alianza kumshambulia Askari na wao walitumia nguvu za kadri lakini aliwatoroka akaenda kuchukua panga, Askari amejeruhiwa vibaya” Kaimu RPC Songwe
“Yule Dereva hakupigwa ilikuwa katika harakati za kumdhibiti na kwa sababu alikuwa anatumia nguvu ndo maana Askari walitumia reasonable force, hakupigwa ila alikuwa anadhibitiwa ili tuweze kumkamata afikishwe ktk Vyombo vya Sheria” Kaimu RPC Songwe
RC Mwanri kaibuka na mpya “kanyaboya hatusaidii we fyeka, hakuna aluatani kunizidi”