Rais John Magufuli amesema wakati anaingia madarakani alikuwa haridhishwi na utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa sababu nchi ilikuwa inaibiwa sana huku baadhi ya Vongozi wa Serikali wakishiriki katika jambo hilo.
Amesema kutokana na jambo hilo aliamua kuutafuta mkataba halisia ambao ulifutwa hususani kipengele cha kukusanya fedha katika makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano hakikuwepo.
“Mwanzoni wakati naingia madarakani sikuridhishwa sana na utendaji wa TCRA, palikuwa na mchezo mbaya sana, tumeibiwa mno, hakuna siri tumechapwa kweli, tumeliwa kweli” Rais Magufuli
“Nikatumia mbinu zangu na Vyombo vya Ulinzi vya Tanzania vinavyojua kuchokoa vizuri sana mkataba original ukapatikana na nikatengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa TCRA Dr. Simba na kupeleka mapendekezo Bungeni ili kukirudisha kile kipengele” Rais Magufuli.