Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndg. Salim Abri Asas leo September 03,2023 ametembelewa na Uongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Taifa (SHIUMA) na Viongozi Mbalimbali wa ngazi ya Mkoa ambapo amesikiliza na kujionea changamoto zinazokabili Machinga Mkoa wa Iringa.
Baada ya kusikiliza kero hizo, MNEC Abri amepokea kwa mikono miwili changamoto zilizowasilishwa na Machinga Mkoani Iringa na ameahidi kushirikiana Bega kwa Bega na SHIUMA Ili kuhakikisha Machinga wanafanya Shughuli zao katika mazingira Bora.
MNEC Abri alipata wasaa wa kutembelea Maeneo mbalimbali ya Machinga na kuzungumza na Machinga ambao wamefurahishwa na kitendo hicho.