Wananchi wa Kilimahewa ‘’B’’ Kata ya Mwanga Kusini katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameamua kuandamana mpaka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakiwa na Mwili wa Mtoto mchanga aliyezaliwa jana na kufariki kwa lengo la kufikisha malalamiko yao kwa RC kufuatia kuzuiwa kumzika kichanga huyo na Mtu aliyedaiwa kufukia kaburi akipinga kutumika kwa eneo lake.
Hata hivyo Wananchi waliamua kumbebesha Mwili huo kutoka eneo la mazishi mpaka kwa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.