Wanachama wa CCM wilaya ya Monduli wameandamana kwenye ofisi za chama hicho wakitaka Mbunge wa CHADEMA Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.
Wakizungumza katika ofisi hizo wamesema wamesikia taarifa za kuteuliwa kwake bila kufuata utaratibu ikiwemo kukaa vikao na wazee wa kimila Malaigwanani ili waweze kumpitisha.
AyoTV na millardayo.com imempata Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Monduli ambaye amesema hajashiriki kwenye vikao na wazee wa kimila kama inavyodaiwa na baadhi ya wanachama hao na kwamba utaratibu utatumika katika kuwapata wagombea.
RC mpya Mbeya alivyotangaza agizo la Rais Magufuli akiapisha “Cheo ni Bahari”