Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umesema utatumia nguvu kuwaondoa wapangaji wanaodaiwa katika nyumba za Serikali na maeneo ya kibiashara endapo wasipo lipa madeni yao ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daudi Kandoro amesema mara baada ya siku 14 kuisha kuanzia leo Juni 1, 2019 watawaondoa Kinguvu wapangaji hao kupitia madalali wa Mahakama.
“Tunasisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada wa kulipa madeni hayo. Pia tumedhamiria kuwafikisha mahakamani wale wote walioondoka/kuondolewa kwenye nyumba kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa na madeni,”
RAIS MAGUFULI ALIVYOTUA KWA MARA YA KWANZA AIRPORT MPYA CHATO