Kijana Fredrick Ochieng mwenye miaka 23 ameuawa na rafiki yake Ian Omondi mwenye miaka 22 kwa kuchomwa na kisu mara mbili, kifuani na tumboni baada ya kunywa bia ya rafiki yake katika baa moja mjini Bondo nchini Kenya.
Kwa mujibu wa uongozi wa Wich-Lum Beach ambapo vijana hao walikuwa wakifanya starehe zao umesema kuwa vijana hao walikuwa wakibishana kabla ya Fredrick kulazimisha kunywa bia ya mwenzake.
Baada ya marehemu kunywa bia ya mwenzake kwa lazima rafiki yake huyo alichomoa kisu na kumchoma kifuani na tumboni Fredrick kitu kilichopelekea marehemu kuanguka chini na kutokwa damu nyingi iliyopelekea kukatisha uhai wake.
Aidha Makamu wa Chief wa eneo hilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Bondo kabla ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Wabunge walivyotamani Kitwanga aongezewe dakika za kuchangia