Daktari Msaidizi wa Hospitali Kuu ya Jeshi la Polisi Kilwa Road, Juma Khalfani (54) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Askari waliojeruhiwa katika maandamano ya CHADEMA walipigwa na kitu chenye ncha kali na Butu.
Dk. Khalifa ambaye ni shahidi wa 5 katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ameyasema hayo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 2, 2019 kwa ajili ya kuendelea na shahidi wa 6.