Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo amekabidhi vitambulisho Milioni moja na laki moja vya awamu ya pili kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogowadogo ambavyo viliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Balozi Kijazi amekabidhi vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Mikoa yote nchini Ikulu DSM na kuwataka Ma-RC kuhakikisha vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wahusika na kwa wakati kwa wahusika na kuongeza kuwa tayari kuna taarifa za baadhi ya watumishi wa Halmashauri ambao wanaviuza vitambulisho hivyo kwa zaidi ya bei elekezi iliyotolea na Rais Magufuli.
Waziri Ummy awajibu wanaosema analitaka Jimbo la Tanga “Mungu akipanga nitapata”