January 14, 2019 Mtanzania Mohamed Mansour Nassor anaetokea Zanzibar akichukua PhD ya Uchumi nchini Urusi ametunukiwa tunzo kubwa ya Kimataifa kwa kuhamasisha vijana wa nchi za Afrika nchini Urusi.
Nassor ni Rais wa Umoja wa Vijana na Wanafunzi wa Nchi zote za Afrika(ASSAFSTU) katika Chuo Kikuu kwa jina maarufu la Patrice Lumumba (RUDN University).
Nassor anatuambia “Kwa heshima kubwa kwangu na kwa nchi yetu, nimetunukiwa Tunzo ya kufanya vyema katika kuhamasisha vijana wa Afrika nchini Urusi katika masuala ya Taaluma na Maendeleo ya Jamii kupitia Shirika la vijana wa Kiafrika lisilo la Kiserikali (NGO) la Youth of Large Exploit(YOLE) katika hafla yao iliofanyika mjini Moscow”
“Leo inakua mara pili kutambuliwa Kimataifa kwa mwaka huu wa 2019 tangu nianze ambapo mwezi huu wa January nilichapishwa na kutambuliwa Kimataifa kama Mtanzania maarufu zaidi katika Watanzania waliowahi kusoma vyuo vya Sovieti ya Urusi na Urusi katika jarida la Kimataifa (Encyclopedia) la Wahitimu wote wa kigeni waliosoma nchini Urusi” Nassor
“Napenda kuwashukuru Watanzania wote wanaounga mkono juhudi zangu na harakati zangu na kwa dua zao njema kwangu hasa kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania linaloongozwa na Raisi Makini kabisa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli” Nassor
RC Mwanri kaibuka na mpya “kanyaboya hatusaidii we fyeka, hakuna aluatani kunizidi”