Mkuu wa Polisi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Debora Hokololo imembidi aitishe kura ya siri kumbaini mhusika wa matukio ya ubakaji wa watoto wadogo wa Shule za Msingi ambavyo vitendo hivyo vikihusishwa na imani za kishirikina.
Matukio hayo ambayo yametokea katika Kitongoji cha Mageuzi katika Kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya ambapo mpaka sasa mtoto mmoja amebakwa na wengine wanne kunusurika kubakwa baada ya kuvua nguo zote na mtu ambaye aliwalazimisha kuvua huku na yeye pia akiwa amevua nguo zake zote.
ACHANA NA NJOMBE MBEYA YAMEIBUKA MAPYA YA KUBAKA UTAJIRIKE